Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjat al-Islam Sheikh Ahmad Qabalan, Mufti mashuhuri wa Ja‘fari wa Lebanon, katika tamko lake alisema:
“Katika hali ngumu zaidi na wakati muhimu zaidi kwa serikali ambao Lebanon imeupitia tangu kuasisiwa kwake, ninaiambia serikali ya Lebanon: Serikali zinabaki hai kwa kujitoa muhanga kiserikali na kwa kulinda uwezo wao wa kitaifa, si kwa kubuni siasa za kukandamiza na kupuuza kujitolea kwa Muqawama muhimu zaidi wa kiserikali katika historia ya dunia ya sasa.”
Akaongeza: kusema “Leo hii, kumbukumbu ya mauaji ya kutisha ya al-Bijar inatukumbusha dhambi ya kuwaacha wale ambao nusu karne iliyopita waliirudisha serikali na nchi, msimamo wetu hapa hautokani na ukaidi au ujasiri, bali unatokana na kusisitiza juu ya umoja wa kitaifa, ushirikiano wa kiraia na maslahi ya kiserikali, na ni ukumbusho usio na shaka kwa ‘hali ya sasa’ kwamba Lebanon bila ya Muqawama wa kipekee isingekuwepo leo.”
Sheikh Qabalan alisema: “Iwapo mshikamano na nchi ya Qatar ni hitaji la ushirikiano, basi mshikamano na watu wa Ghaza wanaouawa mbele ya macho ya ulimwengu wa wastaarabu una umuhimu mkubwa zaidi, wakati umefika serikali ya Lebanon ibebe majukumu yake ya kitaifa kwa ajili ya watu, kusini, Muqawama na chaguo lake la kiserikali. Uadilifu wa kisiasa ni sehemu ya uadilifu wa kiserikali.”
Kiongozi huyu wa Kishia wa Lebanon alieleza kuwa: “Katika muktadha huu, serikali ni yenye dhamana, ni yenye hatia na inalazimika kuonyesha angalau kiwango cha chini cha heshima ya kitaifa na deni la kihistoria ambalo shingo yake imebebeshwa kwa sababu ya Muqawama na deni lake la kipekee, hakuna sauti iliyo juu zaidi kuliko sauti ya heshima ya kibinadamu na kitaifa katika urithi wa Uislamu na Ukristo.”
Akaendelea kusena: “Kukataa mawasiliano ni jambo lililokatazwa, na chuki na uhasama ni makatazo makubwa zaidi, sisi ni kitu kimoja, nchi yetu ni moja, hatari za kieneo ni nyingi sana na hakuna taifa mbadala, yale yaliyotokea na nchi ndugu yetu Qatar yanafichua mchezo hatari wa Marekani katika eneo hili, hakuna tishio lililo kubwa zaidi kwa Lebanon kuliko chuki na uhasama wa kisiasa.”
Sheikh Qabalan alisema: “Nabih Berri ni shakhsia ya kihistoria na ni shakhsia ya kitaifa yenye uwezo wa nadra wa kuleta maridhiano, uongozi na Lebanon hautenganishiki, hakuna mbadala wa kuishi kwa pamoja, mamlaka ya kitaifa, amani ya kiraia na umoja wa milele wetu.”
Na mwisho alisisitiza kwa kusena: “Israeli ni adui wa kiasili, na Muqawama ni nguvu ya Lebanon na uwezo wake wa kipekee wa kusimama imara, makosa yoyote katika uamuzi wa kisiasa yataiweka nchi kwenye kina cha maangamizi.”
Maoni yako